Ayu. 12:23-25 Swahili Union Version (SUV)

23. Huyaongeza mataifa, na kuyaangamiza;Huyaeneza mataifa mbali, na kuyaacha.

24. Huwaondolea moyo wakuu wa watu wa nchi,Na kuwapoteza nyikani pasipokuwa na njia.

25. Wao hupapasa gizani pasipokuwa na mwanga,Naye huwafanya kupepesuka kama vile mlevi.

Ayu. 12