12. Wazee ndio walio na hekima,Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.
13. Hekima na amri zina yeye [Mungu];Yeye anayo mashauri na fahamu.
14. Tazama, yuavunja, wala haiwezekani kujenga tena;Humfunga mtu, wala haiwezekani kumfungua.
15. Tazama, yuayazuia maji, nayo yakatika;Tena, huyapeleka, nayo yaipindua dunia.
16. Kwake yeye ziko nguvu, na makusudi kufanikiwa;Huyo adanganywaye, na mdanganyi pia ni wake.
17. Yeye huwaondoa washauri hali wametekwa nyara,Naye huwafanya waamuzi kuwa ni wapumbavu.
18. Yeye hulegeza kifungo cha wafalme,Na kuwafunga viuno vyao kwa mshipi.