Amo. 2:11-16 Swahili Union Version (SUV)

11. Nami nikawainua watu miongoni mwa wana wenu wawe manabii, na katika vijana wenu wawe Wanadhiri; je! Sivyo hivyo, enyi wana wa Israeli? Asema BWANA.

12. Lakini mliwapa Wanadhiri mvinyo wanywe; mkawaamuru manabii, mkisema, Msifanye unabii.

13. Tazameni, nitawalemea ninyi,Kama gari lilemeavyo lililojaa miganda.

14. Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio;Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake;Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake;

15. Wala apindaye upinde hatasimama;Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka;Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake;

16. Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaaAtakimbia uchi siku ile, asema BWANA.

Amo. 2