Amo. 1:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Maneno ya Amosi, aliyekuwa mmoja wa wachungaji wa Tekoa; maono aliyoyaona katika habari za Israeli, siku za Uzia, mfalme wa Yuda, na siku za Yeroboamu, mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli, miaka miwili kabla ya tetemeko la nchi.

2. Naye alisema,BWANA atanguruma toka Sayuni,Atatoa sauti yake toka Yerusalemu;Na malisho ya wachungaji yataomboleza,Na kilele cha Karmeli kitanyauka.

3. Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya kupuria vya chuma;

Amo. 1