3 Yoh. 1:5-8 Swahili Union Version (SUV)

5. Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao,

6. waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu.

7. Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa.

8. Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.

3 Yoh. 1