1. Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.
2. Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
3. Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.
4. Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.
5. Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali.
6. Yampasa mkulima mwenye taabu ya kazi kuwa wa kwanza wa kupata fungu la matunda.