2 Sam. 7:2-5 Swahili Union Version (SUV)

2. mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.

3. Nathani akamwambia mfalme, Haya, fanya yote yaliyomo moyoni mwako; maana BWANA yu pamoja nawe.

4. Ikawa usiku uo huo, neno la BWANA likamfikia Nathani kusema,

5. Enenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, BWANA asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?

2 Sam. 7