2 Sam. 23:22-38 Swahili Union Version (SUV)

22. Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu.

23. Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake.

24. Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu;

25. na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi;

26. na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi;

27. na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi;

28. na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi;

29. na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini;

30. na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi;

31. na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi;

32. na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani,

33. mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari;

34. na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni;

35. na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi;

36. na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi;

37. na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya;

38. na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri;

2 Sam. 23