2 Sam. 19:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Kisha Yoabu akaambiwa, Angalia, mfalme anamlilia Absalomu na kumwombolezea.

2. Na kushinda kwao vitani siku ile kukageuzwa kuwa maombolezo kwa watu wote; maana watu walisikia siku ile ya kwamba, Mfalme anahuzunika kwa ajili ya mwanawe.

3. Watu wakajificha siku ile, wakaingia mjini kama vile watu waonao fedheha wajifichavyo, hapo wakimbiapo vitani.

4. Mfalme akajifunika uso; na mfalme akalia kwa sauti kuu, Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu!

2 Sam. 19