6. Yule kijana aliyempa habari akasema, Nalikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.
7. Naye alipotazama nyuma, akaniona, akaniita. Nikajibu, Mimi hapa.
8. Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki.
9. Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu.