11. Na baadhi ya Wafilisti walimletea Yehoshafati zawadi, na fedha ya kodi; Waarabu nao wakamletea makundi, kondoo waume saba elfu na mia saba, na mabeberu saba elfu na mia saba.
12. Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina.
13. Naye alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda; na watu wa vita, watu mashujaa humo Yerusalemu.
14. Na hivi ndivyo walivyohesabiwa kwa mbari za baba zao; wa Yuda, maakida wa maelfu; Adna jemadari, na pamoja naye watu mashujaa mia tatu elfu;