2 Fal. 11:19-21 Swahili Union Version (SUV)

19. Akawatwaa wakuu wa mamia, na Wakari, na walinzi, na watu wote wa nchi; wakamleta mfalme kushuka nyumbani mwa BWANA, wakaja kwa njia ya mlango wa walinzi mpaka nyumba ya mfalme. Naye akakaa katika kiti cha enzi cha wafalme.

20. Basi watu wote wa nchi wakafurahi, na mji ukatulia.Naye Athalia wakamwua kwa upanga karibu na nyumba ya mfalme.

21. Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala.

2 Fal. 11