1 Yoh. 5:16-19 Swahili Union Version (SUV)

16. Mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, ataomba, na Mungu atampa uzima kwa ajili ya hao watendao dhambi isiyo ya mauti. Iko dhambi iliyo ya mauti. Sisemi ya kwamba ataomba kwa ajili ya hiyo.

17. Kila lisilo la haki ni dhambi, na dhambi iko isiyo ya mauti.

18. Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.

19. Twajua ya kuwa sisi tu wa Mungu; na dunia yote pia hukaa katika yule mwovu.

1 Yoh. 5