1 Sam. 18:26-28 Swahili Union Version (SUV)

26. Na watumishi wake walipomwambia Daudi; maneno hayo, ilimpendeza Daudi sana kuwa mkwewe mfalme. Na siku zilikuwa hazijaisha bado;

27. basi Daudi akainuka, akaenda yeye na watu wake, akaua katika Wafilisti watu mia mbili; na Daudi akazileta govi zao, wakampa mfalme hesabu kamili, ili awe mkwewe mfalme. Naye Sauli akamwoza Mikali, binti yake.

28. Sauli akaona na kutambua ya kwamba BWANA alikuwa pamoja na Daudi; na huyo Mikali, binti Sauli, akampenda.

1 Sam. 18