1 Nya. 9:34-41 Swahili Union Version (SUV)

34. Hao walikuwa wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, katika vizazi vyao vyote, watu wakuu; nao walikuwa wakikaa huko Yerusalemu.

35. Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, na jina la mkewe aliitwa Maaka;

36. na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni; na Suri, na Kishi, na Baali, na Meri, na Nadabu;

37. na Gedori, na Ahio, na Zekaria, na Miklothi.

38. Na Miklothi akamzaa Shimea. Hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.

39. Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.

40. Na mwana wa Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.

41. Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea.

1 Nya. 9