1 Nya. 8:31-37 Swahili Union Version (SUV)

31. na Gedori, na Ahio, na Zekaria,

32. Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.

33. Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.

34. Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.

35. Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi.

36. Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;

37. na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli;

1 Nya. 8