1 Nya. 7:30-38 Swahili Union Version (SUV)

30. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera.

31. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.

32. Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na umbu lao, Shua.

33. Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti.

34. Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu.

35. Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali.

36. Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra;

37. na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera.

38. Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara.

1 Nya. 7