6. na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni.
7. Na nduguze kwa jamaa zao, hapo ilipohesabiwa nasaba ya vizazi vyao; mkuu wao, Yeieli, na Zekaria,
8. na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hata kufika Nebo na Baal-meoni;
9. na upande wa mashariki akakaa hata kufika maingilio ya jangwa litokalo mto wa Frati; kwa sababu ng’ombe zao walikuwa wameongezeka sana katika nchi ya Gileadi.
10. Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi.
11. Na wana wa Gadi walikuwa wakikaa kwa kuwaelekea, katika nchi ya Bashani mpaka Saleka;
12. Yoeli, alikuwa mkuu wao, na wa pili Shafamu, na Yanai, na Shafati, katika Bashani;