1 Nya. 4:23-30 Swahili Union Version (SUV)

23. Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.

24. Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli;

25. na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma.

26. Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei.

27. Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; walakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kwa mfano wa wana wa Yuda.

28. Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali;

29. na huko Bilha, na Esemu, na Toladi;

30. na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi;

1 Nya. 4