1 Nya. 4:17-20 Swahili Union Version (SUV)

17. Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa.

18. Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.

19. Na wana wa mkewe Hodia, umbu lake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka.

20. Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi.

1 Nya. 4