1 Nya. 27:15-21 Swahili Union Version (SUV)

15. Akida wa kumi na mbili wa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Heledi, Mnetofathi, wa Othnieli; na katika zamu yake walikuwa watu ishirini na nne elfu.

16. Tena wakuu wa kabila za Israeli walikuwa hawa; wa Wareubeni, Eliezeri mwana wa Zikri; wa Wasimeoni, Shefatia mwana wa Maaka;

17. wa Lawi, Hashabia mwana wa Kemueli; wa Haruni, Sadoki;

18. wa Yuda, Elihu, mmojawapo wa nduguze Daudi; wa Isakari, Omri mwana wa Mikaeli;

19. wa Zabuloni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeromothi mwana wa Azrieli;

20. wa wana wa Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia, wa nusu kabila ya Manase, Yoeli mwana wa Pedaya;

21. wa nusu kabila ya Manase katika Gileadi, Ido mwana wa Zekaria; wa Benyamini, Yaasieli mwana wa Abneri;

1 Nya. 27