1 Nya. 25:7-9 Swahili Union Version (SUV)

7. Na hesabu yao, pamoja na ndugu zao waliofundishwa kumwimbia BWANA, wote waliokuwa wastadi, walikuwa mia mbili na themanini na wanane.

8. Wakatupiwa kura ya ulinzi wao, sawasawa wote, mdogo kwa mkubwa, mwalimu kwa mwanafunzi.

9. Kura ya kwanza ikamtokea Yusufu, kwa Asafu; ya pili Gedalia; yeye na nduguze na wanawe, kumi na wawili;

1 Nya. 25