1 Nya. 24:5-14 Swahili Union Version (SUV)

5. Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na wakuu wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.

6. Naye Shemaya, mwana wa Nethaneli, mwandishi, aliyekuwa wa Walawi, akawaandika mbele ya mfalme, na mbele ya wakuu, na Sadoki kuhani, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari, na wakuu wa mbari za baba za makuhani, na za Walawi; ikatwaliwa ya Eleazari mbari moja ya baba, na moja ikatwaliwa ya Ithamari.

7. Kura ya kwanza ikamtokea Yehoiaribu, na ya pili Yedaya;

8. ya tatu Harimu, ya nne Seorimu;

9. ya tano Malkia, ya sita Miyamini;

10. ya saba Hakosi, ya nane Abia;

11. ya kenda Yeshua, ya kumi Shekania;

12. ya kumi na moja Eliashibu, ya kumi na mbili Yakimu;

13. ya kumi na tatu Hupa, ya kumi na nne Yeshebeabu;

14. ya kumi na tano Bilga, ya kumi na sita Imeri;

1 Nya. 24