20. Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya.
21. Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao.
22. Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.
23. Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne.
24. Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri.
25. Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria.
26. Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno.
27. Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri.
28. Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana.
29. Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli.