19. Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
20. Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.
21. Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.
22. Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23. Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.