38. na Obedi akamzaa Yehu; na Yehu akamzaa Azaria;
39. na Azaria akamzaa Helesi; na Helesi akamzaa Eleasa
40. na Eleasa akamzaa Sismai; na Sismai akamzaa Shalumu;
41. na Shalumu akamzaa Yekamia; na Yekamia akamzaa Elishama.
42. Na wana wa Kalebu, nduguye Yerameeli, walikuwa Mesha, mzaliwa wake wa kwanza, aliyekuwa babaye Zifu; na wana wa Maresha, babaye Hebroni.
43. Na wana wa Hebroni; Kora, na Tapua, na Rekemu, na Shema.
44. Naye Shema akamzaa Rahamu, babaye Yorkeamu; na Rekemu akamzaa Shamai.