22. Akisema, Msiwaguse masihi wangu,Wala msiwadhuru nabii zangu.
23. Mwimbieni BWANA, nchi yote;Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
24. Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,Na watu wote habari za maajabu yake.
25. Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana;Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
26. Maana miungu yote ya watu si kitu;Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
27. Heshima na adhama ziko mbele zake;Nguvu na furaha zipo mahali pake.