4. na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;
5. Eluzai, na Yerimothi, na Bealia, na Shemaria, na Shefatia Mharufi;
6. Elkana, na Ishia, na Azaleli, na Yoezeri, na Yashobeamu, Wakora;
7. na Yoela, na Zebadia, wana wa Yerohamu, wa Gedori.
8. Na wa Wagadi wakajitenga kumfuata Daudi ngomeni huko nyikani, waume mashujaa, watu waliozoea vita, walioweza kutumia ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kama nyuso za simba, nao walikuwa wepesi kama kulungu juu ya milima;