4. Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu?
5. Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa.
6. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
7. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
8. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe.