1 Kor. 3:20-23 Swahili Union Version (SUV)

20. Na tena, Bwana anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya kwamba ni ya ubatili.

21. Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu. Kwa maana vyote ni vyenu;

22. kwamba ni Paulo, au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu;

23. nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.

1 Kor. 3