12. Lakini kwa habari za Apolo, ndugu yetu, nalimsihi sana aende kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
13. Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari.
14. Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
15. Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumu watakatifu);
16. watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha.
17. Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu.
18. Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao.