7. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
8. Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
9. mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
10. na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
11. lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.