24. Kwa maana viungo vyetu vilivyo na uzuri havina uhitaji; bali Mungu ameuungamanisha mwili, na kukipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa;
25. ili kusiwe na faraka katika mwili, bali viungo vitunzane kila kiungo na mwenziwe.
26. Na kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote huumia nacho, na kiungo kimoja kikitukuzwa, viungo vyote hufurahi pamoja nacho.
27. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.