1 Kor. 12:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi, ndugu zangu, kwa habari ya karama za roho, sitaki mkose kufahamu.

2. Mwajua ya kuwa mlipokuwa watu wa Mataifa, mlichukuliwa kufuata sanamu zisizonena, kama mlivyoongozwa.

3. Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.

4. Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.

5. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.

1 Kor. 12