1. Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2. wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3. wote wakala chakula kile kile cha roho;
4. wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
5. Lakini wengi sana katika wao, Mungu hakupendezwa nao; maana waliangamizwa jangwani.
6. Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.