1 Fal. 4:13-22 Swahili Union Version (SUV)

13. Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba.

14. Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu.

15. Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani.

16. Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi.

17. Yehoshafati mwana wa Parua, katika Isakari.

18. Shimei mwana wa Ela, katika Benyamini.

19. Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa akida wa pekee katika nchi hiyo.

20. Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.

21. Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.

22. Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori thelathini za unga mzuri, na kori sitini za ngano,

1 Fal. 4