21. akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, BWANA asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya BWANA, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru BWANA, Mungu wako,
22. bali umerudi, ukala chakula ukanywa maji, hapo alipokuambia, Usile chakula, wala usinywe maji; maiti yako haitaliingia kaburi la baba zako.
23. Basi ikawa, alipokwisha kula chakula na kunywa maji, yule nabii aliyemrudisha akamtandikia punda.
24. Na alipokuwa amekwenda zake, simba alimkuta njiani, akamwua. Maiti yake ikatupwa njiani, na yule punda akasimama karibu naye; na yule simba naye akasimama karibu na maiti.