1. Kauli ya Mwenyezi-Mungu:Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadrakibali pia dhidi ya Damasko.Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu,kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli.
2. Hali kadhalika mji wa Hamathi unaopakana na Hadraki;na hata miji ya Tiro na Sidoniingawaje yajiona kuwa na hekima sana.
3. Mji wa Tiro umejijengea ngome kumbwa,umejirundikia fedha kama vumbi,na dhahabu kama takataka barabarani.
4. Lakini Bwana ataichukua mali yake yote,utajiri wake atautumbukiza baharini,na kuuteketeza mji huo kwa moto.