Zekaria 10:10-12 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Nitawarudisha kutoka nchini Misri,nitawakusanya kutoka Ashuru;nitawaleta nchini Gileadi na Lebanoni,nao watajaa kila mahali nchini.

11. Watapitia katika bahari ya mateso,nami nitayapiga mawimbi yake,na vilindi vya maji ya mto Nili vitakauka.Kiburi cha Ashuru kitavunjwana nguvu za Misri zitatoweka.

12. Mimi nitawaimarisha watu wangu,nao watanitii na kuishi kwa kunipendeza.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Zekaria 10