Zaburi 9:2-9 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Nitafurahi na kushangilia kwa sababu yako;nitaliimbia sifa jina lako, ewe Mungu Mkuu.

3. Wakati ulipotokea, maadui zangu walirudi nyuma,walijikwaa na kuangamia.

4. Umenitetea kuhusu kisa changu cha haki;umeketi katika kiti chako cha enzi,ukatoa hukumu iliyo sawa.

5. Umeyakemea mataifa,umewaangamiza waovu;majina yao umeyafutilia mbali milele.

6. Maadui wameangamia milele;umeingolea mbali miji yao,kumbukumbu lao limetoweka.

7. Lakini Mwenyezi-Mungu anatawala milele;ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.

8. Anauhukumu ulimwengu kwa haki;anayaamua mataifa kwa unyofu.

9. Mwenyezi-Mungu ni ngome ya watu wanaoonewa;yeye ni ngome nyakati za taabu.

Zaburi 9