Zaburi 9:15-19 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Watu wa mataifa wametumbukia katika shimo walilochimba,wamenaswa miguu katika wavu waliouficha.

16. Mwenyezi-Mungu amejionesha alivyo;ametekeleza hukumu.Watu waovu wamenaswa kwa matendo yao wenyewe.

17. Waovu wataishia kuzimu;naam, mataifa yote yanayomsahau Mungu.

18. Lakini fukara hawatasahauliwa daima;tumaini la maskini halitapotea milele.

19. Inuka, ee Mwenyezi-Mungu!Usimwache binadamu ashinde.Uyakusanye mataifa mbele yako, uyahukumu.

Zaburi 9