1. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, nakimbilia usalama kwako;uniokoe na wote wanaonidhulumu, unisalimishe.
2. La sivyo, watakuja kunirarua kama simba,wakanivutia mbali, pasiwe na wa kuniokoa.
3. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu!Kama nimetenda moja ya mambo haya:Kama nimechafua mikono yangu kwa ubaya,
4. kama nimemlipa rafiki yangu mabaya badala ya mema,au nimemshambulia adui yangu bila sababu,
5. basi, adui na anifuatie na kunikamata;ayakanyage maisha yangu;na kuniulia mbali.
6. Inuka ee Mwenyezi-Mungu, kwa hasira yako,uikabili ghadhabu ya maadui zangu.Inuka, ee Mungu wangu,wewe umeamuru haki ifanyike.
7. Uyakusanye mataifa kandokando yako,nawe uyatawale kutoka juu.
8. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wayahukumu mataifa;unihukumu kadiri ya uadilifu wangu,kulingana na huo unyofu wangu.