Zaburi 42:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kama paa atamanivyo maji ya kijito,ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!

2. Naona kiu ya Mungu, kiu ya Mungu aliye hai.Nitafika lini kwake na kuuona uso wake?

3. Machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku,waliponiambia kila siku: “Yuko wapi Mungu Wako!”

4. Nakumbuka tena mambo hayakwa majonzi moyoni mwangu:Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu,nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Munguwakipiga vigelegele vya shukrani;umati wa watu wakifanya sherehe!

Zaburi 42