21. Wananishtaki kwa sauti:“Haya! Haya! Tumeona wenyewe uliyotenda!”
22. Lakini wewe Mwenyezi-Mungu waona jambo hilo,usinyamaze, ee Mwenyezi-Mungu,usikae mbali nami.
23. Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu, ukanitetee;uje, ee Mungu wangu, uangalie kisa changu.
24. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, unitetee,ufanye kulingana na uadilifu wako;usiwaache maadui zangu wanisimange.
25. Usiwaache wajisemee: “Tumefanikiwa tulivyotaka!”Au waseme: “Tumemmaliza huyu!”
26. Waache hao wanaofurahia maafa yangu,washindwe wote na kufedheheka.Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi,waone haya na kuaibika.