14. kana kwamba namlilia rafiki au ndugu yangu.Nilikwenda huko na huko kwa huzuni,kama mtu anayeomboleza kifo cha mama yake.
15. Lakini mimi nilipoanguka walikusanyika kunisimanga.Walikusanyika pamoja dhidi yangu.Watu nisiowajua walinirarua bila kukoma,wala hakuna aliyewazuia.
16. Watu ambao huwadhihaki vilema,walinisagia meno yao kwa chuki.
17. Ee Mwenyezi-Mungu, utatazama tu mpaka lini?Uniokoe kutoka kwenye mashambulio yao;uyaokoe maisha yangu na simba hao.
18. Hapo nitakushukuru kati ya kusanyiko kubwa la watu;nitakutukuza kati ya jumuiya kubwa ya watu.