Zaburi 34:8-19 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema.Heri mtu anayekimbilia usalama kwake.

9. Mcheni Mwenyezi-Mungu enyi watakatifu wake;maana wenye kumcha hawatindikiwi na kitu.

10. Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa;lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema.

11. Njoni enyi vijana mkanisikilize,nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu.

12. Je, watamani kufurahia maisha,kuishi maisha marefu na kufurahia mema?

13. Basi, acha kusema mabaya,na kuepa kusema uongo.

14. Jiepushe na uovu, utende mema;utafute amani na kuizingatia.

15. Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu,na kusikiliza malalamiko yao;

16. lakini huwapinga watu watendao maovu,awafutilie mbali kutoka duniani.

17. Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia,na kuwaokoa katika taabu zao zote.

18. Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo;huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.

19. Mateso ya mwadilifu ni mengi,lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote.

Zaburi 34