Zaburi 34:3-13 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu pamoja nami,sote pamoja tulisifu jina lake.

4. Nilimwomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu,na kuniondoa katika hofu zangu zote.

5. Mgeukieni Mungu mpate kufurahi;nanyi hamtaaibishwa kamwe.

6. Maskini alimlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamsikia,na kumwokoa katika taabu zake zote.

7. Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao,na kuwaokoa katika hatari.

8. Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema.Heri mtu anayekimbilia usalama kwake.

9. Mcheni Mwenyezi-Mungu enyi watakatifu wake;maana wenye kumcha hawatindikiwi na kitu.

10. Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa;lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema.

11. Njoni enyi vijana mkanisikilize,nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu.

12. Je, watamani kufurahia maisha,kuishi maisha marefu na kufurahia mema?

13. Basi, acha kusema mabaya,na kuepa kusema uongo.

Zaburi 34