12. Je, watamani kufurahia maisha,kuishi maisha marefu na kufurahia mema?
13. Basi, acha kusema mabaya,na kuepa kusema uongo.
14. Jiepushe na uovu, utende mema;utafute amani na kuizingatia.
15. Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu,na kusikiliza malalamiko yao;
16. lakini huwapinga watu watendao maovu,awafutilie mbali kutoka duniani.
17. Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia,na kuwaokoa katika taabu zao zote.