3. Wakati nilipokuwa sijakiri dhambi yangu,nilikuwa nimedhoofika kwa kulia mchana kutwa.
4. Mchana na usiku mkono wako ulinilemea;nikafyonzwa nguvu zangu,kama maji wakati wa kiangazi.
5. Kisha nilikiri makosa yangu kwako;wala sikuuficha uovu wangu.Nilisema ninakuungamia makosa yangu ee Mwenyezi-Mungu,ndipo nawe ukanisamehe dhambi zangu zote.
6. Kwa hiyo, kila mwaminifu na akuletee maombi;jeshi likaribiapo au mafuriko,hayo hayatamfikia yeye.
7. Wewe ndiwe kinga yangu;wewe wanilinda katika taabu.Umenijalia shangwe za kukombolewa.
8. Mungu asema: “Nitakufunzana kukuonesha njia unayopaswa kufuata.Nitakushauri kwa uangalifu mkubwa.
9. Usiwe mpumbavu kama farasi au nyumbu,ambao lazima wafungwe lijamu na hatamu,la sivyo hawatakukaribia.”