7. Hapo dunia ikatetemeka na kutikisika;misingi ya milima ikayumbayumba,kwani Mungu alikuwa amekasirika.
8. Moshi ulifuka kutoka puani mwake,moto uunguzao ukatoka kinywani mwake;makaa ya moto yalilipuka kutoka kwake.
9. Aliinamisha anga, akashuka chini;na wingu jeusi chini ya miguu yake.
10. Alipanda kiumbe chenye mabawa akaruka;akapaa kasi juu ya mabawa ya upepo.
11. Alijifunika giza pande zote,mawingu mazito yaliyojaa maji yalimzunguka.
12. Umeme ulimulika mbele yake;kukatokea mawinguni mvua ya mawe na makaa ya moto.
13. Mwenyezi-Mungu alinguruma kutoka mbinguni;Mungu Mkuu akatoa sauti yake,kukatokea mvua ya mawe na makaa ya moto.